طه
Twaahaa: 20


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


طه ﴿١﴾
1. Twaahaa


مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ ﴿٢﴾
2. Hatukukuteremshia Qur-aan ili upate mashaka.


إِلَّا تَذْكِرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٣﴾
3. Isipokuwa ni ukumbusho kwa anayekhofu.


تَنزِيلًا مِّمَّنْ خَلَقَ الْأَرْضَ وَالسَّمَاوَاتِ الْعُلَى ﴿٤﴾
4. Ni uteremsho kutoka kwa Yule Aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu kabisa.


الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾
5. Ar-Rahmaan juu ya ‘Arshi Istawaa[1].


لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَمَا تَحْتَ الثَّرَىٰ ﴿٦﴾
6. Ni Vyake Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na vilivyomo baina yake, na vilivyomo chini ya udongo.


وَإِن تَجْهَرْ بِالْقَوْلِ فَإِنَّهُ يَعْلَمُ السِّرَّ وَأَخْفَى ﴿٧﴾
7. Na ukinena kwa jahara; basi hakika Yeye Anajua ya siri na yanayofichika zaidi.


اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Allaah, hapana hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.


وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿٩﴾
9. Na je, imekufikia hadithi ya Muwsaa?


إِذْ رَأَىٰ نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى﴿١٠﴾
10. Alipouona moto akawaambia ahli zake: “Bakieni (hapa); kwa yakini nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo kijinga cha moto, au nipate kwenye huo moto mwongozo.


فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ يَا مُوسَىٰ ﴿١١﴾
11. Basi alipoufikia, aliitwa: “Ee Muwsaa!


إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٢﴾
12. “Hakika Mimi ni Rabb wako; basi vua viatu vyako, kwani wewe hakika uko katika bonde takatifu la Twuwaa.


وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ ﴿١٣﴾
13. “Nami nimekuchagua; basi sikiliza kwa makini yanayofunuliwa Wahy (kwako).


إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي ﴿١٤﴾
14. “Hakika mimi ni Allaah hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru.


إِنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ أَكَادُ أُخْفِيهَا لِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا تَسْعَىٰ ﴿١٥﴾
15. “Hakika Saa itafika tu; Naificha katika ilmu Yangu, ili kila nafsi ilipwe kwa yale iliyoyafanyia juhudi.


فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنْهَا مَن لَّا يُؤْمِنُ بِهَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ فَتَرْدَىٰ ﴿١٦﴾
16. “Basi asikukengeushe nayo yule asiyeiamini na akafuata hawaa, ukaja kuangamia.


وَمَا تِلْكَ بِيَمِينِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿١٧﴾
17. “Na nini hicho kilichokuwemo mkononi mwako wa kuume ee Muwsaa?”


قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّأُ عَلَيْهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَآرِبُ أُخْرَىٰ ﴿١٨﴾
18. (Muwsaa) Akasema: “Hii ni fimbo yangu, naiegemelea, na naangushia majani kwa ajili ya kondoo wangu, na pia nina maarubu mengineyo.”


قَالَ أَلْقِهَا يَا مُوسَىٰ ﴿١٩﴾
19. (Allaah) Akasema: “Basi iangushe ee Muwsaa.”


فَأَلْقَاهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٌ تَسْعَىٰ ﴿٢٠﴾
20. (Muwsaa) Akaiangusha tahamaki hiyo ikawa ni nyoka anayekimbia.


قَالَ خُذْهَا وَلَا تَخَفْ ۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا الْأُولَىٰ ﴿٢١﴾
21. (Allaah) Akasema: “Ichukue na wala usikhofu. Tutairudisha katika hali yake ya awali.


وَاضْمُمْ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ آيَةً أُخْرَىٰ ﴿٢٢﴾
22. “Na ambatisha mkono wako katika ubavu wako, utatoka kuwa mweupe bila ya madhara yoyote; ni Aayah (ishara, dalili) nyingineo. 


لِنُرِيَكَ مِنْ آيَاتِنَا الْكُبْرَى ﴿٢٣﴾
23. “Ili Tukuonyeshe baadhi ya Aayaat (ishara, dalili) Zetu kubwa kabisa.



اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿٢٤﴾
24. “Nenda kwa Fir’awn, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.”


قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي ﴿٢٥﴾
25. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wangu, Nikunjulie kifua changu.


وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي ﴿٢٦﴾
26. “Na niwepesishie shughuli yangu


وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي ﴿٢٧﴾
27. “Na fungua fundo (la kigugumizi) katika lisani yangu.


يَفْقَهُوا قَوْلِي ﴿٢٨﴾
28. “Ili wafahamu kauli yangu.


وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي ﴿٢٩﴾
29. “Na Nifanyie waziri katika ahli zangu.


هَارُونَ أَخِي ﴿٣٠﴾
30. “Haaruwn ndugu yangu.


اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي ﴿٣١﴾
31. “Nitie nguvu kwaye.


وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي ﴿٣٢﴾
32. “Na Umshirikishe katika shughuli yangu.


كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا ﴿٣٣﴾
33. “Ili tukusabbih kwa wingi.


وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا ﴿٣٤﴾
34. “Na tukudhukuru kwa wingi.


إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرًا ﴿٣٥﴾
35. “Hakika Wewe kwetu ni Mwenye kuona.


قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٣٦﴾
36. (Allaah) Akasema: “Umekwishapewa ombi lako ee Muwsaa.


وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَيْكَ مَرَّةً أُخْرَىٰ ﴿٣٧﴾
37. “Na kwa yakini Tulikufanyia ihsaan mara nyingine.


إِذْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰ ﴿٣٨﴾
38. “Tulipomfunulia ilhamu mama yako yale yaliyofunuliwa.


أَنِ اقْذِفِيهِ فِي التَّابُوتِ فَاقْذِفِيهِ فِي الْيَمِّ فَلْيُلْقِهِ الْيَمُّ بِالسَّاحِلِ يَأْخُذْهُ عَدُوٌّ لِّي وَعَدُوٌّ لَّهُ ۚ وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي ﴿٣٩﴾
39. “Kwamba, mtie (Muwsaa) katika sanduku, kisha mtie katika mto (wa Nile). Kisha nao mto utamtupa ufukoni ili amchukue adui Yangu na adui wake (Fir’awn). Na Nikakutilia mahaba kutoka Kwangu, na ili ulelewe Machoni Mwangu.


إِذْ تَمْشِي أُخْتُكَ فَتَقُولُ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ مَن يَكْفُلُهُ ۖ فَرَجَعْنَاكَ إِلَىٰ أُمِّكَ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ ۚوَقَتَلْتَ نَفْسًا فَنَجَّيْنَاكَ مِنَ الْغَمِّ وَفَتَنَّاكَ فُتُونًا ۚ فَلَبِثْتَ سِنِينَ فِي أَهْلِ مَدْيَنَ ثُمَّ جِئْتَ عَلَىٰ قَدَرٍ يَا مُوسَىٰ ﴿٤٠﴾
40. “Alipokwenda dada yako akasema: “Je, nikuelekezeni kwa ambaye atamlea?” Kisha Tukakurudisha kwa mama yako ili yaburudike macho yake, na wala asihuzunike.  Kisha ukaua mtu Tukakuokoa na janga, na Tukakujaribu majaribio mazito. Ukaishi miaka kwa watu wa Madyan, kisha ukaja kama iliyokadiriwa ee Muwsaa.


وَاصْطَنَعْتُكَ لِنَفْسِي ﴿٤١﴾
41. “Na Nimekutayarisha na kukuchagua kwa ajili Yangu ee Muwsaa.


اذْهَبْ أَنتَ وَأَخُوكَ بِآيَاتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكْرِي ﴿٤٢﴾
42. “Nenda wewe na kaka yako kwa Aayaat (ishara, dalili) Zangu, na wala msinyong’onyee katika kunidhukuru.


اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿٤٣﴾
43. “Nendeni wawili nyie kwa Fir’awn, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.

فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ ﴿٤٤﴾
44. “Mwambieni maneno laini, huenda akawaidhika au akakhofu.”


قَالَا رَبَّنَا إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفْرُطَ عَلَيْنَا أَوْ أَن يَطْغَىٰ ﴿٤٥﴾
45. Wakasema: “Rabb wetu! Hakika sisi tunakhofu asije kuharakiza ubaya juu yetu au akapinduka mipaka kuasi.”

قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ ﴿٤٦﴾
46. (Allaah) Akasema: “Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.


فَأْتِيَاهُ فَقُولَا إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ۖ قَدْ جِئْنَاكَ بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكَ ۖوَالسَّلَامُ عَلَىٰ مَنِ اتَّبَعَ الْهُدَىٰ ﴿٤٧﴾
47. “Basi mfikieni, na semeni: “Hakika sisi ni Rasuli wa Rabb wako; basi watume wana wa Israaiyl pamoja nasi, na wala usiwaadhibu. Kwa yakini tumekujia kwa Aayah (ishara, muujiza, dalili) kutoka kwa Rabb wako, na amani iwe juu ya yule atakayefuata mwongozo.


إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿٤٨﴾
48. “Hakika tumefunuliwa Wahy ya kwamba adhabu itakuwa kwa yule atakayekadhibisha na akakengeuka.”

قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ ﴿٤٩﴾
49. (Fir’awn) Akasema: “Basi ni nani Rabb wenu ewe Muwsaa?”


قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾
50. (Muwsaa) Akasema: “Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza.”

قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ ﴿٥١﴾
51. (Fir’awn) Akasema: “Basi nini hali ya karne za awali?”


قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى ﴿٥٢﴾
52. (Muwsaa) Akasema: “Ujuzi wake uko kwa Rabb wangu katika Kitabu. Rabb wangu Hapotezi na wala Hasahau.”


الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّن نَّبَاتٍ شَتَّىٰ ﴿٥٣﴾
53. “Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakupitishieni humo njia, na Akateremsha kutoka mbinguni maji.” Na kwayo Tukatoa aina za mimea mbali mbali.


كُلُوا وَارْعَوْا أَنْعَامَكُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ ﴿٥٤﴾
54.  Kuleni na lisheni wanyama wenu. Hakika katika hayo bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili, zingatio) kwa wenye umaizi.


مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ ﴿٥٥﴾
55. Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.

وَلَقَدْ أَرَيْنَاهُ آيَاتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ ﴿٥٦﴾
56. Na kwa yakini Tulimuonyesha (Fir’awn) Aayaat (ishara, dalili) Zetu zote, lakini alikadhibisha na akakataa kabisa.


قَالَ أَجِئْتَنَا لِتُخْرِجَنَا مِنْ أَرْضِنَا بِسِحْرِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٥٧﴾
57. (Fir’awn) Akasema: “Je, umetujia ili ututoe katika ardhi yetu kwa sihiri yako ewe Muwsaa?”


فَلَنَأْتِيَنَّكَ بِسِحْرٍ مِّثْلِهِ فَاجْعَلْ بَيْنَنَا وَبَيْنَكَ مَوْعِدًا لَّا نُخْلِفُهُ نَحْنُ وَلَا أَنتَ مَكَانًا سُوًى ﴿٥٨﴾
58. “Basi bila shaka tutakuletea sihiri mfano huo; basi tuweke baina yetu na baina yako miadi tusiiendee kinyume sisi na wala wewe, mahali patakapokuwa sawa.”


قَالَ مَوْعِدُكُمْ يَوْمُ الزِّينَةِ وَأَن يُحْشَرَ النَّاسُ ضُحًى ﴿٥٩﴾
59. Akasema: “Miadi yenu ni siku ya mapambo na wakusanye watu wakati wa dhuha.”

فَتَوَلَّىٰ فِرْعَوْنُ فَجَمَعَ كَيْدَهُ ثُمَّ أَتَىٰ ﴿٦٠﴾
60. Basi Fir’awn akageuka, akakusanya hila zake, kisha akaja.



قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيْلَكُمْ لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ ﴿٦١﴾
61. (Muwsaa) Akawaambia: “Ole wenu! Msimtungie Allaah uongo, Akakufutilieni mbali kwa adhabu. Na kwa yakini atashindwa anayetunga uongo.”


فَتَنَازَعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ وَأَسَرُّوا النَّجْوَىٰ ﴿٦٢﴾
62. Wakajadiliana shauri lao baina yao na wakanong’ona kwa siri.



قَالُوا إِنْ هَـٰذَانِ لَسَاحِرَانِ يُرِيدَانِ أَن يُخْرِجَاكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِمَا وَيَذْهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ الْمُثْلَىٰ﴿٦٣﴾
63. Wakasema: “Hakika hawa wawili ni wachawi wanataka kukutoeni katika ardhi yenu kwa sihiri yao na waondoshe mila zenu zilizo kamilifu kabisa.”


فَأَجْمِعُوا كَيْدَكُمْ ثُمَّ ائْتُوا صَفًّا ۚ وَقَدْ أَفْلَحَ الْيَوْمَ مَنِ اسْتَعْلَىٰ ﴿٦٤﴾
64. “Basi jumuisheni hila zenu; kisha fikeni kwa kujipanga safu. Na kwa yakini atafaulu leo atakayeshinda.”

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَلْقَىٰ ﴿٦٥﴾
65. Wakasema: “Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa kwanza kutupa.”


قَالَ بَلْ أَلْقُوا ۖ فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِن سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ ﴿٦٦﴾
66. (Muwsaa) Akasema: “Bali tupeni nyinyi.” Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana kwake kutokana na sihiri yao kwamba zinakwenda mbio.


فَأَوْجَسَ فِي نَفْسِهِ خِيفَةً مُّوسَىٰ ﴿٦٧﴾
67. Basi akahisi khofu katika nafsi yake Muwsaa.


قُلْنَا لَا تَخَفْ إِنَّكَ أَنتَ الْأَعْلَىٰ ﴿٦٨﴾
68. Tukasema: “Usikhofu; hakika wewe ndiye utakayeshinda.”


وَأَلْقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلْقَفْ مَا صَنَعُوا ۖ إِنَّمَا صَنَعُوا كَيْدُ سَاحِرٍ ۖ وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُ حَيْثُ أَتَىٰ ﴿٦٩﴾
69. “Na tupa kile kilichokuweko katika mkono wako wa kulia, kitameza vile walivyoviunda. Hakika walivyoviunda ni hila za mchawi, na wala mchawi hafaulu popote ajapo.”


فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سُجَّدًا قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ هَارُونَ وَمُوسَىٰ ﴿٧٠﴾
70. Basi wachawi wakaangushwa wanasujdu; wakasema: “Tumemwamini Rabb wa Haaruwn na Muwsaa.”



قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ ۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَا أَشَدُّ عَذَابًا وَأَبْقَىٰ ﴿٧١﴾
71. (Fir’awn) Akasema: “Mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu ambaye amekufunzeni sihiri. Basi bila shaka nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha, kisha nitakusulubuni katika mashina ya mitende; na bila shaka mtajua yupi kati yetu ni mkali zaidi wa kuadhibu na wa kudumu.”


قَالُوا لَن نُّؤْثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَاءَنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالَّذِي فَطَرَنَا ۖ فَاقْضِ مَا أَنتَ قَاضٍ ۖ إِنَّمَا تَقْضِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٧٢﴾
72. (Wachawi) Wakasema: “Hatutokukhiyari kuliko ambayo yaliyotujia ya dalili za waziwazi na Yule Aliyetuumba. Basi hukumu unavyotaka kuhukumu, kwani hakika wewe unahukumu (katika) uhai huu wa duniani tu.” 


إِنَّا آمَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغْفِرَ لَنَا خَطَايَانَا وَمَا أَكْرَهْتَنَا عَلَيْهِ مِنَ السِّحْرِ ۗ وَاللَّـهُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿٧٣﴾
73. “Hakika sisi tumemwamini Rabb wetu ili Atughufurie madhambi yetu, na yale uliyotushurutisha katika ya sihiri. Na Allaah ni Mbora Zaidi na Mwenye kudumu zaidi.”


إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿٧٤﴾
74. Hakika yule atayemfikia Rabb wake akiwa mhalifu, basi hakika atapata Jahannam, hatokufa humo na wala hatoishi.


وَمَن يَأْتِهِ مُؤْمِنًا قَدْ عَمِلَ الصَّالِحَاتِ فَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الدَّرَجَاتُ الْعُلَىٰ ﴿٧٥﴾
75. Na yule atakayemfikia akiwa Muumini ametenda mema, basi hao watapata vyeo vya juu.



جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ مَن تَزَكَّىٰ ﴿٧٦﴾
76. Jannaat za milele zipitazo chini yake mitoni wenye kudumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya mwenye kujitakasa.



وَلَقَدْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي فَاضْرِبْ لَهُمْ طَرِيقًا فِي الْبَحْرِ يَبَسًا لَّا تَخَافُ دَرَكًا وَلَا تَخْشَىٰ ﴿٧٧﴾
77. Na kwa yakini Tulimfunulia Wahy Muwsaa kwamba: “Safiri usiku pamoja na waja Wangu, wapigie njia kavu baharini, usikhofu kukamatwa na wala usikhofu (kuzama).”


فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ فَغَشِيَهُم مِّنَ الْيَمِّ مَا غَشِيَهُمْ ﴿٧٨﴾
78. Basi Fir’awn akawafuata pamoja na jeshi lake, yakawafunika humo baharini yaliyowafunika.


وَأَضَلَّ فِرْعَوْنُ قَوْمَهُ وَمَا هَدَىٰ ﴿٧٩﴾
79. Na Fir’awn akawapoteza watu wake, na wala hakuwaongoza.


يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ قَدْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ عَدُوِّكُمْ وَوَاعَدْنَاكُمْ جَانِبَ الطُّورِ الْأَيْمَنَ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ﴿٨٠﴾
80. Enyi wana wa Israaiyl; kwa yakini Tulikuokoeni kutokana na adui wenu; na Tukakuahidini upande wa kulia wa mlima; na Tukakuteremshieni manna na salwaa.


كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَلَا تَطْغَوْا فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبِي ۖ وَمَن يَحْلِلْ عَلَيْهِ غَضَبِي فَقَدْ هَوَىٰ ﴿٨١﴾
81. Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni, na wala msivuke mipaka katika hayo, ikakushukieni ghadhabu Yangu; na itakayemshukia ghadhabu Yangu, basi kwa yakini ameangamia.


وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ ﴿٨٢﴾
82. Na hakika Mimi bila shaka ni Mwingi mno wa kughufuria kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema kisha akaendelea kuongoka.  


وَمَا أَعْجَلَكَ عَن قَوْمِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٨٣﴾
83. “Na nini kilichokuharakisha ukaacha watu wako ee Muwsaa?”


قَالَ هُمْ أُولَاءِ عَلَىٰ أَثَرِي وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ ﴿٨٤﴾
84. (Muwsaa) Akasema: “Hao wako nyuma yangu, na nimeharakiza kukujia Rabb wangu ili Uridhike.”

قَالَ فَإِنَّا قَدْ فَتَنَّا قَوْمَكَ مِن بَعْدِكَ وَأَضَلَّهُمُ السَّامِرِيُّ ﴿٨٥﴾
85. (Allaah) Akasema:  “Basi hakika Tumewatia mtihanini watu wako baada yako, na Saamiriyyu amewapoteza.”



فَرَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَمْ يَعِدْكُمْ رَبُّكُمْ وَعْدًا حَسَنًا ۚ أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ الْعَهْدُ أَمْ أَرَدتُّمْ أَن يَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَخْلَفْتُم مَّوْعِدِي ﴿٨٦﴾
86. Basi Muwsaa akarejea kwa watu wake akiwa ameghadhibika na kusikitika. Akasema: “Enyi watu wangu! Je, Rabb wenu Hakukuahidini ahadi nzuri? Je, imerefuka kwenu ahadi, au mmetaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Rabb wenu, na kwa hiyo mkakhalifu miadi yangu?”


قَالُوا مَا أَخْلَفْنَا مَوْعِدَكَ بِمَلْكِنَا وَلَـٰكِنَّا حُمِّلْنَا أَوْزَارًا مِّن زِينَةِ الْقَوْمِ فَقَذَفْنَاهَا فَكَذَٰلِكَ أَلْقَى السَّامِرِيُّ﴿٨٧﴾
87. Wakasema: “Hatukukhalifu miadi yako kwa khiyari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa na hivyo ndivyo Saamiriyyu alivyoshauri.


فَأَخْرَجَ لَهُمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ فَقَالُوا هَـٰذَا إِلَـٰهُكُمْ وَإِلَـٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ ﴿٨٨﴾
88. Akawaundia ndama kiwiliwili chenye sauti. Wakasema: “Huyu ndiye mwabudiwa wenu na Mwabudiwa wa Muwsaa lakini amesahau (mwabudiwa wake).”


أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ﴿٨٩﴾
89. Je, hawaoni kwamba (huyo ndama) harejeshi neno, na wala hawezi kuwadhuru na wala kuwanufaisha?


وَلَقَدْ قَالَ لَهُمْ هَارُونُ مِن قَبْلُ يَا قَوْمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِ ۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ الرَّحْمَـٰنُ فَاتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوا أَمْرِي﴿٩٠﴾
90. Na Haaruwn alikwishawaambia kabla: “Enyi watu watu! Hakika mmetiwa mtihanini naye (ndama); na hakika Rabb wenu ni Ar-Rahmaan, basi nifuateni na tiini amri yangu.”


قَالُوا لَن نَّبْرَحَ عَلَيْهِ عَاكِفِينَ حَتَّىٰ يَرْجِعَ إِلَيْنَا مُوسَىٰ ﴿٩١﴾
91. Wakasema: “Hatutoacha kumwabudu mpaka arudi kwetu Muwsaa.”


قَالَ يَا هَارُونُ مَا مَنَعَكَ إِذْ رَأَيْتَهُمْ ضَلُّوا ﴿٩٢﴾
92. (Muwsaa aliporejea) Alisema: “Ee Haaruwn! Nini kimekuzuia ulipowaona wanapotoka?


أَلَّا تَتَّبِعَنِ ۖ أَفَعَصَيْتَ أَمْرِي ﴿٩٣﴾
93. “Kwamba unifuate, je, umeasi amri yangu?”


قَالَ يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي ۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَمْ تَرْقُبْ قَوْلِي ﴿٩٤﴾
94. (Haaruwn) Akasema: “Ee mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, na wala kichwa changu. Hakika mimi niliogopa usije kusema: Umefarikisha baina ya wana wa Israaiyl, na wala hukuchunga kauli yangu.”


قَالَ فَمَا خَطْبُكَ يَا سَامِرِيُّ ﴿٩٥﴾
95. (Muwsaa) Akasema: “Una jambo gani ee Saamiriyy?”


قَالَ بَصُرْتُ بِمَا لَمْ يَبْصُرُوا بِهِ فَقَبَضْتُ قَبْضَةً مِّنْ أَثَرِ الرَّسُولِ فَنَبَذْتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتْ لِي نَفْسِي﴿٩٦﴾
96. (Saamirriy) Akasema: “Niliona yale wasiyoyaona na nikateka mteko (wa vumbi) katika kwato za (farasi wa) Jibriyl kisha nikautupa. Na hivyo ndivyo ilivyonishawishi nafsi yangu.”


قَالَ فَاذْهَبْ فَإِنَّ لَكَ فِي الْحَيَاةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَ ۖ وَإِنَّ لَكَ مَوْعِدًا لَّن تُخْلَفَهُ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ إِلَـٰهِكَ الَّذِي ظَلْتَ عَلَيْهِ عَاكِفًا ۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُ فِي الْيَمِّ نَسْفًا ﴿٩٧﴾
97. (Muwsaa) Akasema: “Nenda zako! Kwani hakika utakuwa katika uhai wako kusema: “Usiniguse!” Na hakika una miadi hutovunjiwa. Na mtazame mwabudiwa wako ambaye uliyeendelea kumwabudu. Bila shaka tutamuunguza, kisha tutampeperusha baharini chembechembe.”


إِنَّمَا إِلَـٰهُكُمُ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَسِعَ كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ﴿٩٨﴾
98. “Hakika Mwabudiwa wenu wa haki ni Allaah Ambaye hapana ilaah ila Yeye. Amekienea kila kitu kwa ilimu Yake.”


كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ ۚ وَقَدْ آتَيْنَاكَ مِن لَّدُنَّا ذِكْرًا ﴿٩٩﴾
99. Hivyo ndivyo Tunavyokusimulia miongoni mwa habari zilizotangulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa yakini Tumekupa kutoka Kwetu Ukumbusho.


مَّنْ أَعْرَضَ عَنْهُ فَإِنَّهُ يَحْمِلُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وِزْرًا ﴿١٠٠﴾
100. Atakayejitenga nayo (Qur-aan) basi hakika yeye atabeba Siku ya Qiyaamah mzigo (wa dhambi).


خَالِدِينَ فِيهِ ۖ وَسَاءَ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حِمْلًا ﴿١٠١﴾
101. Ni wenye kudumu humo (motoni), na mzigo mbaya ulioje kwao kuubea Siku ya Qiyaamah.


يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ وَنَحْشُرُ الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ زُرْقًا ﴿١٠٢﴾
102. Siku itakayopulizwa katika baragumu. Na Tutawakusanya wahalifu Siku hiyo hali macho yao yatakuwa rangi ya buluu (kwa kiwewe).


يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا ﴿١٠٣﴾
103. Wakinong'onezana baina yao: “Hamkukaa (duniani) isipokuwa (siku) kumi tu.”


نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا ﴿١٠٤﴾
104. Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyasema; atakaposema mbora wao katika mwendo: “Hamkukaa isipokuwa siku moja tu.”


وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا ﴿١٠٥﴾
105. Na wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu majabali. Sema: “Rabb wangu Atayapeperusha chembechembe.”


فَيَذَرُهَا قَاعًا صَفْصَفًا ﴿١٠٦﴾
106. “Kisha Ataiacha ardhi kuwa tambarare, uwanda ulio sawasawa.”


لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجًا وَلَا أَمْتًا ﴿١٠٧﴾
107. Hutoona humo mdidimio wala mwinuko. 


يَوْمَئِذٍ يَتَّبِعُونَ الدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُ ۖ وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا ﴿١٠٨﴾
108. Siku hiyo watamfuata mwitaji hakuna kumkengeuka; na sauti zitafifia kwa Ar-Rahmaan, basi hutosikia isipokuwa mchakato wa nyayo.


يَوْمَئِذٍ لَّا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَرَضِيَ لَهُ قَوْلًا ﴿١٠٩﴾
109. Siku hiyo haitofaa shafaa’ah isipokuwa wa yule Atakayepewa idhini na Ar-Rahmaan na Akamridhia kusema.


يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾
110.  Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha ujuzi Wake.


وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا ﴿١١١﴾
111. Nyuso zitanyenyekea kwa Aliye Hai daima, Msimamizi wa kila kitu. Na kwa yakini ameharibikiwa abebaye dhulma.


وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا يَخَافُ ظُلْمًا وَلَا هَضْمًا ﴿١١٢﴾
112. Na yeyote atakayetenda mema naye ni Muumini, basi hatokhofu dhulma wala kupunjwa.


وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا وَصَرَّفْنَا فِيهِ مِنَ الْوَعِيدِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ أَوْ يُحْدِثُ لَهُمْ ذِكْرًا ﴿١١٣﴾
113. Na hivyo ndivyo Tumeiteremsha Qur-aan kwa Kiarabu, na Tukaisarifu waziwazi humo vitisho kadhaa, huenda wakapata kuwa na taqwa au ikawapa makumbusho. 


فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا﴿١١٤﴾
114. Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Na wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: “Rabb wangu! Nizidishie elimu.”


وَلَقَدْ عَهِدْنَا إِلَىٰ آدَمَ مِن قَبْلُ فَنَسِيَ وَلَمْ نَجِدْ لَهُ عَزْمًا ﴿١١٥﴾
115. Na kwa yakini Tulimpa Aadam ahadi kabla, lakini akasahau, na wala Hatukuona kwake azimio.


وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ ﴿١١٦﴾
116. (Na taja) Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa kabisa.


فَقُلْنَا يَا آدَمُ إِنَّ هَـٰذَا عَدُوٌّ لَّكَ وَلِزَوْجِكَ فَلَا يُخْرِجَنَّكُمَا مِنَ الْجَنَّةِ فَتَشْقَىٰ ﴿١١٧﴾
117. Tukasema: “Ee Aadam! Hakika huyu (Ibliys) ni adui wako na wa mkeo, basi angalieni asikutoeni katika Jannah ukapata mashaka.”


إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعْرَىٰ ﴿١١٨﴾
118. “Hakika wewe humo hutopata njaa, na wala hutokuwa uchi.”


وَأَنَّكَ لَا تَظْمَأُ فِيهَا وَلَا تَضْحَىٰ ﴿١١٩﴾
119. “Na kwamba wewe hutopata kiu humo, na wala hutopigwa na joto la jua”


فَوَسْوَسَ إِلَيْهِ الشَّيْطَانُ قَالَ يَا آدَمُ هَلْ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ الْخُلْدِ وَمُلْكٍ لَّا يَبْلَىٰ ﴿١٢٠﴾
120. Lakini shaytwaan alimtia wasiwasi, akasema: “Ee Aadam! Je, nikuelekeze mti wa kudumu na ufalme usiochakaa.”


فَأَكَلَا مِنْهَا فَبَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۚ وَعَصَىٰ آدَمُ رَبَّهُ فَغَوَىٰ﴿١٢١﴾
121. Basi waliula, uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Jannah. Na Aadam akamuasi Rabb wake akapotoka.


ثُمَّ اجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَتَابَ عَلَيْهِ وَهَدَىٰ ﴿١٢٢﴾
122. Kisha Rabb wake Akamteua, Akapokea tawbah yake na Akamwongoza.



قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ ﴿١٢٣﴾
123. (Allaah) Akasema: “Teremkeni humo nyote, hali ya kuwa maadui nyinyi kwa nyinyi. Kisha utakapokufikieni kutoka Kwangu Mwongozo, basi atakayefuata Mwongozo Wangu, hatopotea na wala hatopata mashaka.”


وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ﴿١٢٤﴾
124. “Na atakayejitenga na ukumbusho Wangu basi hakika atapata maisha ya dhiki, na Tutamfufua Siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu.”


قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا ﴿١٢٥﴾
125. Atasema: “Rabb   wangu! Kwa nini Umenifufua kipofu, na hali nilikuwa naona?”



قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ ﴿١٢٦﴾
126. (Allaah) Atasema: “Hivyo ndivyo, zilikufikia Aayaat Zetu ukazisahau   na kadhaalika leo umesahauliwa.”


وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي مَنْ أَسْرَفَ وَلَمْ يُؤْمِن بِآيَاتِ رَبِّهِ ۚ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبْقَىٰ ﴿١٢٧﴾
127. Na kadhaalika Tutakavyomlipa yule anayevuka mipaka na asiamini Aayaat za Rabb wake. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kali zaidi na ni ya kudumu zaidi.


أَفَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ﴿١٢٨﴾
128. Je, haikuwa mwongozo kwao (kujua) karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao, na wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo bila shaka ni Aayaat (zingatio, mawaidha) kwa wenye kumaizi.


وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامًا وَأَجَلٌ مُّسَمًّى ﴿١٢٩﴾
129. Na ingekuwa si neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako, na muda uliokadiriwa, bila shaka ingelazimika (adhabu hapa duniani).


فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ وَمِنْ آنَاءِ اللَّيْلِ فَسَبِّحْ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرْضَىٰ ﴿١٣٠﴾
130. Basi subiri juu ya yale wanayoyasema, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua, na kabla kukuchwa kwake. Na katika nyakati za usiku pia sabbih na katikati ya mchana huenda ukapata ya kukuridhisha.


وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٣١﴾
131. Na wala usikodolee macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, hayo ni mapambo ya uhai wa dunia tu, ili Tuwajaribu kwayo. Na riziki ya Rabb wako ni bora zaidi na ni yenye kudumu zaidi.


وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿١٣٢﴾
132. Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha kusubiri kwayo. Hatukuombi riziki. Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.


وَقَالُوا لَوْلَا يَأْتِينَا بِآيَةٍ مِّن رَّبِّهِ ۚ أَوَلَمْ تَأْتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٣٣﴾
133. Na (makafiri) wakasema: “Kwanini hatuletei Aayah (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb wake?” Je, kwani haikuwafikia hoja bayana zilokuwemo katika Sahifa za awali? 


وَلَوْ أَنَّا أَهْلَكْنَاهُم بِعَذَابٍ مِّن قَبْلِهِ لَقَالُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ مِن قَبْلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخْزَىٰ ﴿١٣٤﴾
134. Na lau Tungeliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: “Rabb wetu! Kwa nini Usituleteee Rasuli tukafuata Aayaat Zako kabla hatujadhalilika na hatujahizika?”


قُلْ كُلٌّ مُّتَرَبِّصٌ فَتَرَبَّصُوا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ أَصْحَابُ الصِّرَاطِ السَّوِيِّ وَمَنِ اهْتَدَىٰ ﴿١٣٥﴾
135. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Kila mmoja ni mwenye kungojea na kutazamia, basi ngojeeni na tazamieni, karibuni mtajua ni nani mwenye njia iliyo sawa na ni nani aliyeongoka.”