الْكَهْف
Al-Kahf: 18
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۜ﴿١﴾
1. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Ambaye Amemteremshia mja Wake (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu na wala Hakukifanya ndani yake kiwe kombo.
قَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِّن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا ﴿٢﴾
2. Kimenyooka sawa ili Awaonye adhabu shadidi kutoka Kwake (Allaah), na kiwabashirie Waumini ambao wanatenda mema kwamba watapata ujira mzuri.
مَّاكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا ﴿٣﴾
3. Wakae humo abadi.
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ﴿٤﴾
4. Na kiwaonye wale wanaosema (kuwa) Allaah Amejifanyia mwana.
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا ﴿٥﴾
5. Hawana elimu yoyote kwayo na wala baba zao. Neno kubwa linatoka katika midomo yao. Hawasemi isipokuwa uongo tu.
فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا ﴿٦﴾
6. Basi huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa ghamu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya athari zao za kutokuamini Hadithi hii (Qur-aan.).
إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ﴿٧﴾
7. Hakika Sisi Tumefanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili Tuwajaribu nani miongoni mwao mwenye ‘amali nzuri kabisa.
وَإِنَّا لَجَاعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا ﴿٨﴾
8. Na hakika Sisi bila shaka Tutafanya vilivyo juu yake kuwa udongo wenye ukame.
أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا ﴿٩﴾
9. Je, unadhani kwamba watu wa pangoni na maandiko walikuwa miongoni mwa Aayaat (miujiza, ishara) Zetu za ajabu?
إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا ﴿١٠﴾
10. Pale vijana walipokimbilia katika pango wakasema: “Rabb wetu! Tupe kutoka Kwako rahmah, na Tutengenezee katika jambo letu mwongozo wa sawa.”
فَضَرَبْنَا عَلَىٰ آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا ﴿١١﴾
11. Basi Tukawaziba masikio yao pangoni (kuwalaza) kwa idadi ya miaka mingi.
ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ أَيُّ الْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوا أَمَدًا ﴿١٢﴾
12. Kisha Tukawainua ili Tujue nani kati ya makundi mawili lilohesabu madhubuti zaidi kuhusuu muda wao waliobakia.
نَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى ﴿١٣﴾
13. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) habari zao kwa haki. Hakika wao ni vijana waliomwamini Rabb wao; na Tukawazidishia Uongofu.
وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَن نَّدْعُوَ مِن دُونِهِ إِلَـٰهًا ۖ لَّقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا ﴿١٤﴾
14. Na Tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama wakasema: “Rabb wetu, ni Rabb wa mbingu na ardhi. Hatutomuomba muabudiwa asiyekuwa Yeye, kwani yakini hapo tutakuwa tumesema kauli ya kufuru ya kuvuka mpaka.
هَـٰؤُلَاءِ قَوْمُنَا اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ لَّوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِم بِسُلْطَانٍ بَيِّنٍ ۖ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ﴿١٥﴾
15. Hawa watu wetu wamejichukulia waabudiwa pasi Naye. Kwa nini hawaleti juu yao hoja bayana? Basi nani dhalimu zaidi kuliko anayemtungia Allaah uongo?
وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ﴿١٦﴾
16. Na mlipokuwa mmejitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Allaah; basi kimbieni pangoni; Rabb wenu Atakufungulieni rahmah Zake, na Atakutengenezeeni wepesi katika jambo lenu.”
وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِّنْهُ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ ۗ مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا﴿١٧﴾
17. Na ungeliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia; na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto, nao wamo katika uwazi wa humo. Hiyo ni miongoni mwa Aayaat (miujiza, ishara) za Allaah. Ambaye Allaah Amemwongoza, basi yeye ndiye aliyeongoka. Na Anayempotoa basi hutompatia mlinzi wa kumuongoza.
وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ ۚ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ ۖ وَكَلْبُهُم بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ ۚلَوِ اطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا ﴿١٨﴾
18. Na utawadhania wamacho na hali wao wamelala. Na Tunawagueza upande wa kulia na upande wa kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeliwatazama, bila shaka ungegeuka na kuwakimbia, na bila shaka ungejazwa tisho kubwa juu yao.
وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَاهُمْ لِيَتَسَاءَلُوا بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ قَالُوا رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَابْعَثُوا أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَـٰذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَا أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا ﴿١٩﴾
19. Na hivyo ndivyo Tulivyowainua usingizini ili waulizane baina yao. Msemaji miongoni mwao akasema: “Muda gani mmekaa?” Wakasema: “Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.” Wakasema: “Rabb wenu Anajua zaidi muda mliokaa. Basi tumeni mmoja wenu mjini kwa noti hizi atazame chakula chake kipi kifaacho zaidi kisha akuleteeni chakula hicho. Na awe makini na busara na wala asikutambulisheni kwa yeyote.”
إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا ﴿٢٠﴾
20. “Hakika wao wakikugundueni, watakupigeni mawe au watakurudisheni katika mila zao; na hapo hamtofaulu abadani.
وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِم بُنْيَانًا ۖ رَّبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا ﴿٢١﴾
21. Na hivyo ndivyo Tulivyowatambulisha kwa watu ili wajue kwamba ahadi ya Allaah ni haki. Na kwamba Saa haina shaka yoyote humo pale walipozozana baina yao kuhusu jambo lao. Wakasema: “Jengeni jengo juu yao; Rabb wao Anawajua vyema.” Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: “Bila shaka tutajenga msikiti juu yao.”
سَيَقُولُونَ ثَلَاثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًا بِالْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَاءً ظَاهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا ﴿٢٢﴾
22. Watasema: “Watatu na wanne wao ni mbwa wao.” Na (wengine) wanasema: “Watano na wa sita wao ni mbwa wao” - kwa kuvurumisha bila ya kujua. Na (wengine) wanasema: “Saba na wa nane wao ni mbwa wao.” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Rabb wangu Anajua zaidi idadi yao.” Hakuna anayewajua isipokuwa wachache tu. Basi usibishane nao isipokuwa mabishano dhahiri (Tuliyokufunilia Wahy), na wala usimuulize yeyote kuhusu habari zao.
وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا ﴿٢٣﴾
23. Na wala usiseme kamwe kwa jambo lolote “Nitalifanya hilo kesho.”
إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ وَاذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّي لِأَقْرَبَ مِنْ هَـٰذَا رَشَدًا ﴿٢٤﴾
24. Isipokuwa In Shaa Allaah. Na mdhukuru Rabb wako unaposahau. Na sema: “Asaa Rabb wangu Akaniongoa njia iliyo karibu zaidi na uongofu kuliko hii.”
وَلَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَازْدَادُوا تِسْعًا ﴿٢٥﴾
25. Na walikaa pangoni mwao miaka mia tatu na wakazidisha tisa.
قُلِ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا ۖ لَهُ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَبْصِرْ بِهِ وَأَسْمِعْ ۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِي حُكْمِهِ أَحَدًا ﴿٢٦﴾
26. Sema: “Allaah Anajua zaidi muda waliokaa. Ni Yake Pekee ghayb za mbingu na ardhi. Kuona kulioje Kwake na kusikia! Hawana pasi Naye mlinzi yeyote na wala Hamshirikishi katika hukumu Zake yeyote.
وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا ﴿٢٧﴾
27. Na soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy katika Kitabu cha Rabb wako. Hakuna yeyote atakayeweza ubadilisha Maneno Yake; na wala hutopata kamwe makimbilio isipokuwa Kwake.
وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾
28. Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akakafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka.
وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا ۚ وَإِن يَسْتَغِيثُوا يُغَاثُوا بِمَاءٍ كَالْمُهْلِ يَشْوِي الْوُجُوهَ ۚ بِئْسَ الشَّرَابُ وَسَاءَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٢٩﴾
29. Na sema: “Hii ni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru.” Hakika Sisi Tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka. Na wakiomba uokozi watapewa maji kama masazo ya zebaki nyeusi ziliyoyeyushwa yanayobabua nyuso. Ubaya ulioje kinywaji hicho, na uovu ulioje mahali pa kupumzikia.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ﴿٣٠﴾
30. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa anayetenda ‘amali nzuri kabisa.
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۚ نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٣١﴾
31. Hao watapata Jannaat za milele zipitazo chini yao mito, watapambwa humo vikuku vya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri laini na hariri nzito nyororo; wakiegemea humo kwenye makochi ya fakhari. Uzuri ulioje wa thawabu na mahali pazuri palioje pa kupumzikia.
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا ﴿٣٢﴾
32. Na wapigie mfano wa watu wawili. Tulimjaalia mmoja wao bustani mbili za mizabibu, na Tukazizungushia kwa mitende, na Tukaweka baina yake mimea.
كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِم مِّنْهُ شَيْئًا ۚ وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا ﴿٣٣﴾
33. Bustani zote mbili zilitoa mazao yake, na wala hazikupunguza humo chochote. Na Tukabubujua baina yake mito.
وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا ﴿٣٤﴾
34. Naye akawa ana mazao. Akasema kwa sahibu yake naye huku akijadili naye: “Mimi nina mali zaidi kuliko wewe, na mwenye nguvu zaidi kwa idadi ya watu.”
وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِ أَبَدًا ﴿٣٥﴾
35. Akaingia bustanini mwake hali naye amejidhulumu nafsi yake akasema “Sidhani kama haya yatatoweka abadani.”
وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا ﴿٣٦﴾
36. “Na wala sidhani kama Saa (Qiyaamah) itasimama; na hata kama nitarudishwa kwa Rabb wangu, bila shaka nitakuta marejeo bora kuliko haya.”
قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا ﴿٣٧﴾
37. Sahibu yake akamwambia na huku anajadiliana naye: “Je, umemkufuru Yule Aliyekuumba kutokana na mchanga, kisha kutokana na manii, kisha Akakusawazisha kuwa mtu?
لَّـٰكِنَّا هُوَ اللَّـهُ رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِرَبِّي أَحَدًا ﴿٣٨﴾
38. Lakini (mimi naamini) Yeye Allaah Ndiye Rabb wangu; na wala sitomshirikisha Rabb wangu na yeyote.
وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ إِن تَرَنِ أَنَا أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا ﴿٣٩﴾
39. Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Maa Shaa Allaah! Hapana nguvu ila za Allaah. Japo kama unaniona mimi nina mali na watoto kidogo kuliko wewe?
فَعَسَىٰ رَبِّي أَن يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِّنَ السَّمَاءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا﴿٤٠﴾
40. Basi asaa Rabb wangu Akanipa yaliyo bora kuliko bustani yako, na Akaipelekea kudura ya maafa kutoka mbinguni; ikapambazukiwa kuwa tambarare inayoteleza.
أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْرًا فَلَن تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَبًا ﴿٤١﴾
41. Au yakawa maji yake ya kudidimia kisha hutoweza kuyafuatilia.”
وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَا أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا ﴿٤٢﴾
42. Basi mazao yake yakazungukwa (na maangamizi), akabakia anapindua pindua viganja vyake (kusikitika) juu ya yale aliyoyagharamia humo, nayo yameporomoka juu ya chanja zake; na huku anasema: “Laiti nisingelimshirikisha Rabb wangu na yeyote.”
وَلَمْ تَكُن لَّهُ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا ﴿٤٣﴾
43. Na hakuwa ana kundi lolote la kumnusuru pasina Allaah, na wala hakuweza kujisaidia.
هُنَالِكَ الْوَلَايَةُ لِلَّـهِ الْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا ﴿٤٤﴾
44. Huko (Aakhirah) utawala ni wa Allaah Pekee wa haki. Yeye ni Mbora zaidi wa kulipa thawabu, na Mbora zaidi wa matokeo ya mwisho.
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾
45. Na wapigie mfano wa uhai wa dunia kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika kwayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha yakawa makavu yaliyovurugika yanapeperushwa na pepo. Na Allaah daima juu ya kila kitu ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa.
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾
46. Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini.
وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾
47. Na Siku Tutayoyaendesha majabali na utaiona ardhi tambarare tupu, na Tutawakusanya; Hatutomwacha hata mmoja katika wao.
وَعُرِضُوا عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا﴿٤٨﴾
48. Na watatandazwa mbele ya Rabb wako safu safu; (Allaah Atasema): “Kwa yakini mmetujia kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza. Bali mlidai kwamba Hatukukuwekeeni miadi (hii).”
وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾
49. Na kitawekwa Kitabu, basi utaona wahalifu ni wenye khofu kwa yale yaliyokuwemo ndani yake; na watasema: “Ole wetu! Kitabu hiki kina nini, hakiachi dogo wala kikubwa isipokuwa kimerekodi hesabuni.” Na watakuta yale waliyoyatenda yamehudhuria. Na Rabb wako Hamdhulumu yeyote.
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا ﴿٥٠﴾
50. Na (taja) pale Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikuwa miongoni mwa majini akaasi amri ya Rabb wake. Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake walinzi, pasi Nami; na hali wao kwenu ni maadui? Ubaya ulioje mbadala kwa madhalimu.
مَّا أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ الْمُضِلِّينَ عَضُدًا ﴿٥١﴾
51. (Allaah Anasema): “Sikuwashuhudisha kuumbwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa nafsi zao; na wala Sikuwa Mwenye kuwachukua wapotoshaji wa kunitia nguvu.”
وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا شُرَكَائِيَ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا ﴿٥٢﴾
52. Na Siku Tutakayosema: “Iteni washirika mliodai (ni waungu). Watawaita, lakini hawatowaitikia; na Tutaweka baina yao mahali pa maangamizi.
وَرَأَى الْمُجْرِمُونَ النَّارَ فَظَنُّوا أَنَّهُم مُّوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا عَنْهَا مَصْرِفًا ﴿٥٣﴾
53. Na wahalifu watauona moto, watajua hakika kwamba wao ni wenye kuangukia humo, na hawatopata kutoka humo njia ya kuepuka.
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا ﴿٥٤﴾
54. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna katika hii Quraan kwa watu, kwa kila mifano. Lakini binaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.
وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا ﴿٥٥﴾
55. Na hakuna kilichowazuia watu kuamini ulipowajia Mwongozo na wakamwomba maghfirah Rabb wao isipokuwa iwafikie desturi ya watu wa awali, au iwafikie adhabu ya kuwakabili.
وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۚ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ ۖوَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنذِرُوا هُزُوًا ﴿٥٦﴾
56. Na Hatukutuma Rusuli isipokuwa wabashiriaji na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabisha kwa batili ili watengue haki kwa batili hiyo. Na wakazichukua Aayaat (na ishara) Zangu na yale waliyoonywa nayo kuwa ni mzaha.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ ۚ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۖ وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا ﴿٥٧﴾
57. Na Nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayaat za Rabb wake, akazipuuza na akayasahu yale iliyotanguliza mikono yake. Hakika Sisi Tumeweka nyoyoni mwao vifuniko wasizifahamu (Aayaat), na katika masikio yao uziwi. Na ukiwaita kwenye mwongozo hawataongoka abadani!
وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ ۚ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا مِن دُونِهِ مَوْئِلًا ﴿٥٨﴾
58. Na Rabb wako ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye Rahmah. Kama Angeliwachukulia kwa yale waliyoyachuma, Angeliwaharakizia adhabu. Bali wao wana miadi, hawatopata pasi Naye kimbilio la kuepukana nayo.
وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا ﴿٥٩﴾
59. Na hiyo ni miji Tuliyoiangamiza walipodhulumu; na Tukafanya miadi kwa maangamizo yao.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ﴿٦٠﴾
60. Na (taja) pale Muwsaa alipomwambia kijana wake: “Sitaacha kuendelea mpaka nifikie zinapokutana bahari mbili, na nitaendelee muda mrefu.”
فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا ﴿٦١﴾
61. Basi walipofika zinapoungana bahari mbili, walimsahau samaki wao; naye akachukua njia yake baharini akiporonyoka.
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبًا ﴿٦٢﴾
62. Walipokwishapita; alimwambia kijana wake: “Tuletee chakula chetu cha mchana; tumekwishapata machofu katika hii safari yetu.”
قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ ۚ وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا ﴿٦٣﴾
63. (Kijana wake) Akasema: “Unaona pale tulipopumzika katika jabali. Basi mimi nilimsahau samaki; na hakunisahaulisha isipokuwa shaytwaan nisimkumbuke; akachukua njia yake baharini kimaajabu.”
قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ ۚ فَارْتَدَّا عَلَىٰ آثَارِهِمَا قَصَصًا ﴿٦٤﴾
64. (Muwsaa) Akasema: “Hapo ndipo tulipokuwa tunapataka.” Basi wakarudi nyuma kwa kufuata athari za nyayo zao.
فَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا ﴿٦٥﴾
65. Wakamkuta mja miongoni mwa waja Wetu (Khidhr), Tuliyempa rahmah kutoka Kwetu, na Tumemfunza kutoka kwetu elimu.
قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ﴿٦٦﴾
66. Muwsaa akamwambia: “Je, nikufuate ili unifunze katika yale uliyofunzwa ya busara?”
قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٦٧﴾
67. (Khidhr) Akasema: “Hakika hutoweza kustahamili pamoja nami.
وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا ﴿٦٨﴾
68. Na vipi utastahamili kwa ambayo huyaelewi vyema utambuzi wake?”
قَالَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا ﴿٦٩﴾
69. (Muwsaa) Akasema: “Utanikuta In Shaa Allaah mwenye subira na wala sitokuasi amri.”
قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَن شَيْءٍ حَتَّىٰ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا ﴿٧٠﴾
70. (Khidhr) Akasema: “Basi utakaponifuata, usiniulize kuhusu lolote mpaka nianze kukutajia.”
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا ﴿٧١﴾
71. Basi wakatoka kuendelea kwenda, mpaka walipopanda jahazi. (Khidhr) akaipasua. Akasema: “Umeitoboa ili ugharikishe watu wake? Kwa yakini umeletea jambo zito la munkari!”
قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٧٢﴾
72. (Khidhr) Akasema: “Je, sikusema kwamba hakika wewe hutoweza kustahamili pamoja nami?”
قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا ﴿٧٣﴾
73. (Muwsaa) Akasema: “Usinichukulie kwa niliyoyasahau, na wala usinifanyie tashdidi kubwa kwa jambo langu hili.”
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُّكْرًا ﴿٧٤﴾
74. Basi wakatoka kuendelea kwenda, mpaka wakakutana na ghulamu. akamuua. (Muwsaa) Akasema: “Umeua nafsi iliyotakasika asiyekuwa na kosa la kuua nasfi? Kwa yakini umeleta jambo linalokirihisha mno lisilokubalika!
قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٧٥﴾
75. (Khidhr) Akasema: “Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutoweza kustahamili pamoja nami?”
قَالَ إِن سَأَلْتُكَ عَن شَيْءٍ بَعْدَهَا فَلَا تُصَاحِبْنِي ۖ قَدْ بَلَغْتَ مِن لَّدُنِّي عُذْرًا ﴿٧٦﴾
76. (Muwsaa) Akasema: “Nikikuuliza kuhusu chochote baada ya haya; basi usisuhubiane nami, maana umekwishapata udhuru kwangu.”
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا أَتَيَا أَهْلَ قَرْيَةٍ اسْتَطْعَمَا أَهْلَهَا فَأَبَوْا أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُ ۖ قَالَ لَوْ شِئْتَ لَاتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا ﴿٧٧﴾
77. Basi wakatoka kuendelea kwenda, mpaka wakawafikia watu wa mji wakawaomba watu wake chakula; lakini wakakataa kuwakaribisha. Wakakuta humo ukuta unataka kuanguka; basi (Khidhr) akausimamisha. (Muwsaa) Akasema: “Ungelitaka bila shaka ungeliichukulia ujira.”
قَالَ هَـٰذَا فِرَاقُ بَيْنِي وَبَيْنِكَ ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٧٨﴾
78. (Khidhr) Akasema: “Huku ndiko kufarikiana baina yangu na baina yako. Hivi karibuni nitakujulisha tafsiri ya hakika ya yale uliyoshindwa kuyavutia subira.”
أَمَّا السَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَاكِينَ يَعْمَلُونَ فِي الْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَاءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا ﴿٧٩﴾
79. “Ama jahazi, ilikuwa ya masikini wanaofanya kazi baharini. Basi nikataka kuitia dosari kwani mbele yao alikuweko mfalme anayechukua kila jahazi kwa kupora.”
وَأَمَّا الْغُلَامُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَا أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَانًا وَكُفْرًا ﴿٨٠﴾
80. “Na ama ghulamu, walikuwa wazazi wake wawili Waumini. Basi Tukakhofu asiwatie mashakani kwa upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru.”
فَأَرَدْنَا أَن يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِّنْهُ زَكَاةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا ﴿٨١﴾
81. “Tukakusudia Rabb wao Awabadilishie aliye bora zaidi kuliko yeye aliyetakasika na aliyekuwa karibu zaidi kihuruma.”
وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٨٢﴾
82. “Na ama ukuta, ulikuwa ni wa ghulamu wawili mayatima katika mji ule, na kulikuweko chini yake hazina yao, na mzazi wao alikuwa mwema. Basi Rabb wako Alitaka wafikie umri wa kupevuka na watoe hazina yao, ni rahmah kutoka kwa Rabb wako. Na sikufanya hayo kwa amri yangu. Hiyo ni tafsiri ya hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavutia subira.”
وَيَسْأَلُونَكَ عَن ذِي الْقَرْنَيْنِ ۖ قُلْ سَأَتْلُو عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا ﴿٨٣﴾
83. Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnayn. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nitakusomeeni kuhusu baadhi ya habari zake.”
إِنَّا مَكَّنَّا لَهُ فِي الْأَرْضِ وَآتَيْنَاهُ مِن كُلِّ شَيْءٍ سَبَبًا ﴿٨٤﴾
84. Hakika Sisi Tulimmakinisha katika ardhi, na Tukampa njia ya kila kitu.
فَأَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٨٥﴾
85. Basi akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِي عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ قُلْنَا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِمَّا أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّا أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا ﴿٨٦﴾
86. Hata alipofika machweo ya jua; Magharibi, akalikuta linatua katika chemchemu ya matope meusi (au ya moto), na akakuta huko watu. Tukasema: “Ee Dhul-Qarnayn! Ima uwaadhibu au wafanyie ihsaan”
قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوْفَ نُعَذِّبُهُ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِ فَيُعَذِّبُهُ عَذَابًا نُّكْرًا ﴿٨٧﴾
87. (Dhul-Qarnayn) Akasema: “Ama aliyedhulumu, basi Tutamuadhibu, kisha atarudishwa kwa Rabb wake, Amuadhibu adhabu kali kabisa ya kukirihisha, isiyovumilika.”
وَأَمَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُ جَزَاءً الْحُسْنَىٰ ۖ وَسَنَقُولُ لَهُ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا ﴿٨٨﴾
88. “Na ama aliyeamini na akatenda mema, basi atapata jazaa nzuri. Na Tutamwambia yaliyo mepesi katika amri Yetu.”
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٨٩﴾
89. Kisha akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَىٰ قَوْمٍ لَّمْ نَجْعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتْرًا ﴿٩٠﴾
90. Hata alipofikia panapochomza jua (Mashariki), akalikuta linachomoza kwa watu Hatukuwafanyia kizuizi cha kuwakinga nalo.
كَذَٰلِكَ وَقَدْ أَحَطْنَا بِمَا لَدَيْهِ خُبْرًا ﴿٩١﴾
91. Ndio hivyo. Na Tulikwishazijuia vyema habari zote zilizokuwa pamoja naye.
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٩٢﴾
92. Kisha akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا ﴿٩٣﴾
93. Hata alipofikia baina ya milima miwili akakuta nyuma yao watu ambao hawakaribii kufahamu kauli yoyote.
قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا ﴿٩٤﴾
94. Wakasema: “Ee Dhul-Qarnayn! Hakika Ya-juwj na Ma-juwj ni mafisadi katika ardhi, basi je, tukufanyie ujira ili uweke baina yetu na baina yao kizuizi?”
قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا ﴿٩٥﴾
95. Akasema: “Alivyonimakinisha Rabb wangu ni bora zaidi (kuliko ujira), basi nisaidieni kwa nguvu (za watu) niweke baina yenu na baina yao kizuizi imara.”
آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انفُخُوا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا ﴿٩٦﴾
96. “Nileteeni vipande vya chuma. Mpaka aliposawazisha kujaza baina ya kingo mbili za majabali; akasema: “Pulizeni.” Hata alipovifanya moto, akasema: “Nipeni nimwagie juu yake shaba iliyoyayushwa.”
فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا ﴿٩٧﴾
97. Basi (Ya-juwj na Ma-juwj) hawakuweza kuukwea, na wala hawakuweza kuutoboa.
قَالَ هَـٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّي ۖ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ ۖ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا ﴿٩٨﴾
98. (Dhul-Qarnayn) Akasema: “Hii ni Rahmah kutoka kwa Rabb wangu. Basi itakapokuja ahadi ya Rabb wangu, Ataujaalia obomoke, upondeke uwe tambarare. Na ahadi ya Rabb wangu daima ni ya kweli.
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ ۖ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا ﴿٩٩﴾
99. Na siku hiyo Tutawaacha wasongamane kama mawimbi wenyewe kwa wenyewe. Na litapulizwa baragumu, Tutawakusanya wote katika mkusanyo mmoja.
وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِّلْكَافِرِينَ عَرْضًا ﴿١٠٠﴾
100. Na siku hiyo Tutahudhurisha Jahannam kwa ajili ya makafiri kuonyeshwa waziwazi.
الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَن ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا ﴿١٠١﴾
101. Ambao macho yao yalikuwa katika pazia kutokana na kutokunidhukuru na walikuwa hawawezi kusikia (Aayaat kuwatia iymaan).
أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِن دُونِي أَوْلِيَاءَ ۚ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا ﴿١٠٢﴾
102. Je wanadhania wale waliokufuru kwamba wanaweza kuchukua waja Wangu kuwa walinzi badala Yangu? Hakika Sisi Tumeandaa Jahannam kwa ajili ya makafiri kuwa mahala pa kuteremkia.
قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾
103. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, Tukujulisheni wenye kukhasirika mno kwa ‘amali?”
الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾
104. Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia, na huku wao wakidhani kwamba wanapata mazuri kwa matendo yao.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾
105. Hao ni wale waliozikanusha Aayaat (na ishara) za Rabb wao na kukutana Naye basi zimeporomoka ‘amali zao; hivyo Hatutowasimamishia Siku ya Qiyaamah uzito wowote.
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ﴿١٠٦﴾
106. Hivyo ndio jazaa yao Jahannam kwa yale waliyoyakufuru na kuchukulia mzaha Aayaat (na ishara) Zangu na Rusuli Wangu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ﴿١٠٧﴾
107. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, watapata Jannaat za Al-Firdaws kuwa ni mahali pao pa makaribisho.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا ﴿١٠٨﴾
108. Ni wenye kudumu humo hawatotaka kuihama.
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا﴿١٠٩﴾
109. Sema: “Kama bahari ingelikuwa ni wino wa (kuandika) maneno ya Rabb wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Rabb wangu, japokuwa Tungelileta mfano wake kujaza tena.
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾
110. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee. Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende ‘amali njema na wala asishirikishe yeyote katika ‘ibaadah za Rabb wake”
0 Comments